Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Inthaasharia (TIC), Taifa Samaahat Sheikh Hemedi Jalala, jana katika ziara yake ndefu ya kutembelea vituo mbali mbali vya Jumuiya hiyo nchini Tanzania, alifanya ufunguzi rasmi wa Ofisi ya (TIC) Mkoani hapo. Sheikh Jalala takriban mara moja kila mwaka amekuwa na ada hiyo ya kutembelea vituo mbali mbali ambavyo vipo chini ya mwamvuli wa (TIC), ili kujua changamoto ambazo zinavikabili vituo hivyo na kufanya usahili wa baadhi ya vituo vyengine.
Sambamba na tukio hilo Sheikh huyo huku akiambatana na ujumbe wake pia waliweza kuhudhuria kwenye hafla maalumu ya Maulidi ya Mtume Muhammad (saww) yaliyo andaliwa na sheikh Kabeke ambae ni sheikh wa Mkoa wa Mwanza BAKWATA.
Picha za tukio kamili ni kama ifuatavyo:
Maoni yako